Abstract:
Tendi za Kiswahili zimekuwepo katika maeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki tangia
karne ya 17 na zimekuwa zikienziwa, kudhaminiwa na kusawiri tamaduni na asasi z
a
wakazi hawa. Uwepo wa tendi katika maeneo ya Kiafrika uliwahi kuzua mjadala
mkubwa kutoka kwa wasomi wa Kimagharibi waliodai kuwa Afrika hakuna tendi ila
kinachodaiwa kuitwa tendi ni masimulizi ya kisifo tu. Wengine wamezifutilia mbali tendi
hizi kwa kud
ai kuwa maudhui yake ni ya kichawi na sihiri. Ukweli ni kwamba, utafiti
uliofanywa na watafiti hawa uliegemea mitazamo ya Kimagharibi. Licha ya kuwa
kuliibuka watafiti waliodai kuwa hakuna tofauti kati ya tendi za maeneo haya mawili,
hakujafanywa utafiti l
inganishi wa kutathmini ujitokezaji wa vipengele vya kimaumbo na
motifu katika tendi za Kiswahili za Kiafrika na zile za Kimagharibi zilizotafsiriwa kwa
lugha ya Kiswahili. Madhumuni makuu yalikuwa ni kuhakiki maumbo yanayobainika
baina ya tendi za Kiafrik
a na zile za Kimagharibi. Mtafiti alinuia kuchunguza tendi mbili
zinazopatikana katika maeneo ya Kiafrika na Kimagharibi. Tendi hizi ni
Utendi wa
Mikidadi na Mayasa
unaopatikana Afrika na
katika maeneo ya Kimagharibi
Utendi wa Kalevala
unaopatikana Finland
. Mtafiti alichunguza tendi hizi mbili kutoka eneo la Afrika
na Kimagharibi kwa sababu zina upekee katika mitindo na fani, zinabeba historia ya
kipekee katika maeneo yao, zinaibua motifu mbalimbali na zinafungamana na
madhumuni ya utafiti huu. Utafiti huu
uliongozwa na nadharia mbili kuu ambazo ni
Nadharia ya Umtindo iliyoasisiwa na Barry na Nadharia ya Ruwaza ya Shujaa
iliyoasisiwa na mwanafalsafa Joseph Campbell. Mihimili ya nadharia hizi ilitumiwa na
mtafiti kueleza upeo na mipaka ya utafiti huu na pia
ilisaidia kuchanganua data. Utafiti
huu ulihusisha kusoma makala na kutumiwa kama data ya utafiti huu ambayo baadaye
ilichanganuliwa na mwishowe kuelezea matokeo kwa kutumia mbinu ya kimaelezo.
Utafiti huu pia ulihusisha ukusanyaji wa data moja kwa moja ku
toka maktabani. Mahali
pa utafiti palikuwa ni maktaba na sampuli ya utafiti huu ilikuwa
Mayasa
unaopatikana Afrika na
Utendi wa Kalevala
Utendi wa Mikidadi na
unaopatikana maeneo ya
Kimagharibi uliotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Matokeo ya utafiti ya
libaini kuwa
vipengele vya kimaumbo, motifu na changamoto zinazowakumba majagina zilizobainika
katika tendi za Kiafrika zilidhihirika pia katika tendi za Kimagharibi. Inatarajiwa kuwa
utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kwa jamii ya wasomi hasa wanaoshu
ghulikia
fasihi linganishi na utajaribu kutatua ubishi ulioko kuhusu tendi za maeneo mbalimbali.
Utafiti huu pia utasaidia kuhifadhi tendi za Kiswahili.